Sunday, December 27, 2009

Mtumia

Ulezi,
Mimi siuwezi,
Kisa, wema hautengenezi,
Uovu haupunguzi,
Umezidi ubazazi,
Kukiri ya upuzi,
Si jana wala juzi,
Hayo ndiyo yako makaazi,
Kashindwa wako mzazi,
Aliye na zaidi mapenzi,
Nimefanya upelelezi,
Sitopata mageuzi,
Ndio maana siyaulizi,
Siniteue kwenye hii kazi,
Nina zangu pingamizi,
Siifanyi hata kwa hirizi,
Unayo mwenyewe mageuzi,
Fanya hima upekuzi,
Mtumia ulile hilo andazi!

Labels

poetry (10)